HabariK24 TvSwahiliSwahili VideosTop StoriesVideos

Sakata ya NCPB: Ni hasara kwa waliovuna mahindi Trans Nzoia, Uasin Gishu

Huku sakata ya wakiritimba wachache kulipwa mabilioni ya pesa kutokana na kufikisha mahindi yao katika shirika la nafaka na mazao ikiendelea kutokota, maelfu ya wakulima katika eneo la kaskazini mwa bionde la ufa wanazidi kusononeka na maelfu ya magunia ya mahindi ambayo wameshindwa kuuza.
Wakulima hao wanasema kuwa licha ya kufikisha mahindi yao katika maghala ya NCPB, shirika hilo lilichukua kiasi kidogo cha mahindi na kuwarejesha nyumbani na magunia mengi ya mahindi , ambayo baadhi yake yameanza kuoza.

Show More

Related Articles