HabariPilipili FmPilipili FM News

Kaunti Ya Kilfi Yatajwa Kuongoza Kwa Visa Vya Dhuluma Za Kijinsia.

Serikali kupitia wizara ya jinsia na maswala ya vijana nchini sasa imesama kunahaja ya washikadau pamoja na viongozi mbali mbali kushirikiana ili kupunguza visa vya dhuluma za kijinsia kwa wasichana wilioko chini ya umri wa miaka kumi na 18.

Kulingana na katibu katika wizara ya jinsia Recheal Shebesh kwa sasa kaunti ya kilfi inaongoza kwa visa vya dhuluma kwa wasichana chini ya umri wa 18.

Shebesh amesema tabia ya ubakaji na wasichana wadogo kuingizwa kwenye ngono na mimba za mapema ndio chanzo cha ugonjwa wa Kasuri maarufu Fistula.

Kauli yake imeungwa mkono na mwakilishi wa wanawake kaunti ya kilifi Getrude Mbeyu ambaye amasema kuwa anashirikana na asasi za usalama ili kuhakikisha watoto walioko chini ya umri wa mika 18 hawapatikani kwa sherehe za usiku.

Show More

Related Articles