HabariK24 TvSwahiliSwahili VideosVideos

Sonko kusalia Machakos hadi ahakikishiwe usalama 

Serikali kupitia kwa wizara ya usalama wa ndani imepuuzilia mbali madai ya Gavana wa Nairobi Mike Sonko kwamba maisha yake yamo hatarini.

Haya yanajiri baada ya kubainika kwamba Sonko amekuwa akiwafanyia kazi wakazi wa Nairobi kutoka nyumbani kwake kaunti ya Machakos ambapo wizara hiyo imemtaka kukomesha sokomoko zinazoshuhudiwa.

Kwa upande wake Gavana Sonko kwenye mahojiano na runinga ya K24 amesema Nairobi harudi ng’o hadi pale usalama wake utakapoimarishwa.

Wizara ya usalama wa ndani aidha imekanusha madai kwamba Sonko amesalia na mlinzi mmoja na kusema ana walinzi watano kama magavana wengine.

Show More

Related Articles