HabariK24 TvSwahiliSwahili VideosTop StoriesVideos

Mama aliyejifungua asalia na sindano kwenye sehemu za siri, Bungoma

Visa vya masihara ya madaktari dhidi ya wagonjwa wao wakati wa upasuaji vimekuwa vikigonga vichwa vya habari katika siku za hivi majuzi.

Cha hivi punde kikiwa kisa kinachomhusisha mama wa miaka 18 ambapo madaktari walimfanyia upasuaji ili kumsaidia kujifungua na kisha kusahau sindano ya kumshona katika sehemu zake za siri.

Kwa siku 13 sasa mama huyo aliyefanyiwa upasuaji huo katika zahanati ya Bulondo kaunti ya Bungoma amekuwa akikabiliana na uchungu baada ya juhudi za kutoa sindano hiyo kukatizwa uharibifu wa mashine iliyopaswa kuwaelekeza madaktari ilikokuwa sindano hiyo.

Mwanamke huyo hata hivyo tayari amefanyiwa upasuaji hii leo na sindano hiyo kutolewa.

Show More

Related Articles