HabariMilele FmSwahili

IPOA yaanzisha uchunguzi kuhusu madai ya polisi kumuua mwanamke katika bustani ya City Nairobi

Mamlaka ya kuangazia utendakazi wa polisi IPOA imeanzisha uchunguzi kuhusu madai ya polisi kuwauwa mwanamke na mwanaume katika bustani ya City Park hapa Nairobi kwa kuwamiminia risasi jumapili iliyopita. Uchunguzu wa IPOA unakwenda sambamba na ule wa idara ya jinai ambayo tayari imeanzisha uchunguzi dhidi ya maafisa hao. Mkurugenzi wa mawasiliano wa IPOA Dennis Oketch amedhibitisha kuwa maafisa wa IPOA wanalenga kubaini kiini cha mauaji hayo na kupendekeza kuchukuliwa hatua maafisa hao iwapo watagundulika kukiuka sheria. Uchunguzi wa awali umebaini kuwa polisi hao wa utawala William Chir Chir kutoka kituo cha polisi cha Makadara na Godfrey Kitui kutoka kituo cha Industrial Area waliwapiga risasi na kuwauwa Janet waiyaki wa miaka 41 papo hapo huku mwathiriwa mwengine Bernard Chege akikimbizwa hospitali.

Show More

Related Articles