HabariMilele FmSwahili

Uchukuzi wakatizwa Murang’a baada ya barabara ya Kanjama Kiria-Ini Kangema kuporomoka

Uchukuzi umekatizwa katika kaunti ya Muranga baada ya sehemu ya bara bara ya Kanjama Kiria-Ini Kangema kuporomoka. Mamlaka ya bara bara za mashambani KERRA inasema hali hiyo imesababishwa na maporomoko ya ardhi. KERRA imewashauri madereva kutumia bara bara mbadala huku suluhu likisakwa. Yakijiri hayo takribani familia 200 zimeachwa bila makao katika kijiji cha Kawainda kaunti ya Kiambu baada ya nyumba zao zaidi ya 20 kufurika. famili hizo zinaitaka serikali ya kaunti ya Kiambu kukarabati mabomba ya maji taka ili kuepusha athari zaidi za mafuriko.

Show More

Related Articles