HabariMilele FmSwahili

Moto wateketeza chumba cha kujifungulia kina mama katika hospitali ya Mbagathi

Akina mama wajawazito waliojifungua na wanao wachanga wamesalia kuhangaika katika hospitali ya Mbagathi hapa Nairobi baada ya chumba cha kujifungua kushika moto usiku wa kuamkia leo. Ingawa hakuna aliyejeruhiwa katika tukio hilo,inadaiwa waathiriwa hao walitolewa haraka huku maafisa hospitalini humo wakiuzima moto huo. Chumba hicho cha kujifungua akina mama kinadaiwa kujengwa mwaka 2014 na ni mwezi jana tuu ambapo wahandisi walilitaja jengo hilo kama lisilokuwa salama

Show More

Related Articles