HabariMilele FmSwahili

DPP Noordin Haji aahidi kushughulikia msongamano wa wafungwa magerezani

Kiongozi wa mashtaka ya umma Noordin Haji ameahidi kushughulikia msongamano wa wafungwa walio magerezani. Akiongea huko Nakuru Noordin anasema atazindua awamu ya pili ya kuangazia kesi zilizoko mahakamani. Uchunguzi waliofanya kwenye vituo 10 vya rumande na kuhojiwa washukiwa 4000 washukiwa 13 wamekuwa rumande kwa kati ya miaka 7 hadi 10 wakisubiri kukamilika kwa kesi zao. Anasema 86 hawakuwa na uwezo wa kulipia thamana. Usemi wake unafuatia lalama za wafungwa wanaodai kucheleweshwa kwa kesi zao.

Show More

Related Articles