HabariMilele FmSwahili

Kongamano la ugatuzi la mabunge ya kaunti na seneti laingia siku ya pili leo Mombasa

Kongamano la ugatuzi la mabunge ya kaunti na seneti litaendelea leo huko Mombasa baada ya kufunguliwa rasmi na naibu wa rais William Ruto hapo jana. Waakilishi walitumia mkao wa hapo jana kushinikiza kutengewa hazina maalum ya kuwawezesha kutekeleza majukumu yao. Suala lingini lililoangaziwa na naibu wa rais ni kutaka bunge la seneti kusaidia kubuni sheria za kudhibiti kesi nyingi zinazochipuka kwenye kaunti na kupelekea kupotea kwa fedha nyingi zinazotumika kwenye kesi hiyo. Kinara wa ODM Raila Odinga anatazamiwa kufunga rasmi kongamano hilo hapo kesho.

Show More

Related Articles