HabariPilipili FmPilipili FM News

Wanachama wa ICPK Watakao Patikana Na Hatia Ya Ufujaji Wa Pesa Za Umma Kuchukuliwa Hatua Kali

Kongamano la 34 la Taasisi ya wahasibu wa umma nchini ICPK limengoa nanga rasmi  hapa mjini Mombasa.

Akizungumza katika uzinduzi  wa kongamano hilo mwenyekiti wa taasisi hiyo Julius mwatu, ameapa  kuwachukulia hatua kali mahasibu waliojisajili  na taasisi hiyo, na ambao watapatikana na hatia ya ufujaji wa pesa katika shirika la vijana kwa taifa NYS.

Kwa upande wake  Nelson Gaichuhie ambaye ni katibu katika wizara ya  fedha ,amewataka wahasibu kuwajibika zaidi katika kazi zao akisema hatua hiyo itasaidia pakubwa kufanikisha ajenda nne kuu za serikali.

Show More

Related Articles