HabariK24 TvSwahiliSwahili VideosTop StoriesVideos

Zaidi ya washukiwa 30 wa sakata ya NYS kufikishwa kortini wiki hii

Washukiwa zaidi wa sakata ya shilingi bilioni 9 katika shirika la huduma ya vijana kwa taifa NYS hii leo walizidi kumiminika katika makao makuu ya upelelezi wa jinai walikohojiwa kuhusiana na ufujaji wa mabilioni ya pesa.
K24 saa moja imebaini kuwa baadhi yao watafunguliwa mashtaka kortini kabla ya kutamataika kwa wiki hii.
Aidha imebainika kwamba baadhi ya washukuiwa hao waliohusika na ufujaji wa mali ya umma tayari wanakaguliwa kimaisha ilikubaini iwapo walijitajirisha kiharamu.
Vile vile, washukiwa hao wamepokonywa magari ya kifahari na hata baadhi ya majengo wanayomiliki.

Show More

Related Articles