HabariMilele FmSwahili

Serikali yakata rufaa dhidi ya uamuzi wa kumuachilia huru kasisi Ng’ang’a

Mkurungenzi wa mashitaka ya umma Noordin Haji amekata rufaa dhidi ya uamuzi wa mahakama ya Kiambu kumuachilia huru kasisi James Ng’ang’a. Kasisi Nganga pamoja na watu wengi wane wanakabiliwa na tuhuma za kuhusika katika mauaji ya mwanamke kuopitia uendeshaji mbaya wa gari waliachiliwa na hakimu Godfrey Oduor, majuma mawili yaliyopita kutokana na kile akilitaja kuwa ushahidi kukumbwa na hitilafu nyingi. Polisi walishutumiwa kwa kutoendesha uchunguzi kabambe hali iliyopelekea kesi ya nganga kutupiliwa mbali.

Show More

Related Articles