HabariMilele FmSwahili

Watu 34 wadhibitishwa kufariki kutokana na athari za mafuriko kaunti ya Kitui

Watu 34 wamedhibitishwa kufariki kutokana na athari za mafuriko katika kaunti ya Kitui. Kaunti kamishena wa Kitui Samuel Kimiti anasema kwamba maafisa wa kaunti hiyo wanaendelea kukusanya takwimu zaidi kutoka maeneo mbali mbali ya kaunti kubaini idadi kamili ya walioangamia.

Kadhalika kimiti amewataka wakazi wa maeneo ya Kyuso karibu na mto Tana kuhamia sehemu salama hasaa baada ya bwawa la Masinga kujaa kutokana na mvua kubwa inayoendelea kunyesha

Show More

Related Articles