HabariMilele FmSwahili

Shughuli za usafiri zatatizika baada ya barabara kadhaa nchini kuporomoka

Shughuli za usafiri zimeripotiwa kutatizika leo barabara kadhaa nchini zikiporomoka. Barabara ya Iten-Kabarnet inadaiwa kupata mipasuko, hali sawia imeshuhudiwa barabara za Lodwar -Kakuma kaunti ya Turkana sawa barabara ya Mandera kuelekea Rhamu pamoja na Nyeri-Othaya. Yakijiri hayo naibu rais William Ruto pamoja na waziri wa ugatuzi Eugene Wamalwa wanatarajiwa alasiri hii eneo la Garsen kaunti ya Tanariver kuongoza zoezi la kuwapa misaada waathiriwa wa mafuriko. Ujio wao ukiwadia huku wenyeji wakilalamikia ukokefu wa bidhaa muhimu kama vile dawa na vyoo

Show More

Related Articles