HabariMilele FmSwahili

Aliyekuwa waziri wa uchukuzi Micheal Kamau kuwashtaki maafisa wa EACC

Aliyekua waziri wa uchukuzi Michael Kamau anaelekea mahakamani kuwashtaki maafisa wa tume ya EACC waliovamia makao yake mtaani Karen hapa Nairobi mapema leo. Wakili wake Nelson Havi anasema msako huo ulifanywa kinyume na sheria kwani mahakama ya rufaa ilitoa agizo la kuzuia uchunguzi wa aina yeyote kwa mteja wake. Amelaumu EACC kwa kukiuka maagizo ya mahakama akisema kesi ya utumizi mbaya wa afisi iliokua inamkabili kamau ilitupiliwa mbali na mahakama.
Kamau aliyejiuzulu mwaka 2015 anakabiliwa na kosa la kushawishi utoaji wa kandarasi ya ujenzi wa barabara ya Kamukuywa-Kaptama-Kapsokwony-Sirisia iliopewa kampuni ya Engiconsult Limited kwa gharama ya shilingi milioni 33.3.

Show More

Related Articles