HabariMilele FmSwahili

Naibu rais afungua rasmi kongamano la mabunge ya kaunti na seneti Mombasa

Naibu wa rais William Ruto anafungua rasmi kongamano la mabunge ya kaunti na seneti huko Mombasa. Wengine wanaohudhuria kongamano hilo la 3 ni spika wa bunge la seneti Ken Lusaka, mwenyekiti wa baraza la magavana Josphat Nanok na waziri wa ugatuzi Euegne Wamalwa. Ni mkao utakaotumika kulainisha shughuli za mabunge ya kaunti katika kubuni sheria za kufanikisha ugatuzi,suala la kufurushwa kwa magavana pia litajadiliwa. Kinara wa ODM Raila Odinga anatazamiwa kuhutubia mkao huo katika hafla ya kuufunga siku ya Alhamisi.

Show More

Related Articles