HabariPilipili FmPilipili FM News

Wanafunzi Wa Vyuo Vikuu Na Wale Wa Taasisi Za Kiufundi Kupata Ufadhili. Kwale

Jumla ya shilingi milioni 5 zimetolewa kufadhili masomo kwa wanafunzi wa vyuo vikuu na wale wa taasisi za kiufundi katika gatuzi dogo la matuga kaunti ya kwale .
Mbunge wa Matuga kassim sawa tandaza aliyekua akizungumza wakati wa kupeana hundi hiyo Katika afisi za CDF mjini Kwale amesema ametenga jumla ya shilingi millioni 10 za kufadhili masomo ya vyuo kwa wanafunzi werevu wanaotoka katika jamii zisizo bahatika eneo la matuga kama njiamoja ya kuimarisha viwango vya elimu na maendeleo katika jamii za eneo hilo .
Tandaza amekiri kukithiri kwa umaskini miongoni mwa jamii za Matuga kuchangiwa na ukosefu wa elimu ya kutosha jambo analosema limesambaratisha pakubwa uchumi na maendeleo katika eneo hilo.

Show More

Related Articles