HabariMilele FmSwahili

Mwanamme asombwa na maji eneo la Lugari kaunti ya Kakamega

Mwanamme mmoja amesombwa na maji ya mafuriko alipojaribu kuvuka mto Nambirima uko Lugari kaunti ya Kakamega. Wenyeji wanasema marehemu kwa jina Mwangi Kirau alisombwa na maji baada ya kufurika kwa mto huo. Kwa sasa shughuli za kusaka mwili wake zinaendelea. Wametaka serikali ya kaunti ya Kakamega kukarabati barabara hiyo wanayosema imeaharibiwa na mvua.

Show More

Related Articles