HabariPilipili FmPilipili FM News

Wafanyikazi Wa Soka la Ibiza Watalazimika Kuhamia Katika Uwanja Wa Maonesho Ya Kilimo Wa Ukunda.

Wafanyibiashara  wa soko la Ibiza  huko Ukunda Kwale wanasema bado hawajapata mwelekeo mwafaka wa  eneo  watakalo fanyia biashara zao, baada ya soko la Ibiza kuvunjwa na halmashauri ya barabara  KeNHA  ili kutoa nafasi ya upanuzi wa barabara  kuu ya Likoni –Lungalunga.

Christine Mbuvi mfanyibiashara wa mboga katika soko hilo anasema hatua hio imewafanya kutoleta bidhaa nyingi  wakihofia  kufurushwa kwa mara ya pili katika soko la Ibiza ambapo wanaendeleza biashara zao kwa muda.

Mwenyekiti wa soko hilo  Omar Bakari amethibitisha kuwa serikali ya kaunti imewatengea  wafanyibiashara hao eneo la uwanja wa maonyesho ya kilimo  la ukunda  hivyo watalazimika kuhamia huko kufikia siku ya jumatano baada ya muda wa mwezi mmoja waliopewa  na KeNHA kulihama soko la Ibiza  kukamilika  siku ya jumamosi .

Show More

Related Articles