HabariPilipili FmPilipili FM News

Idadi Ya Wanafunzi Wanao Jiunga Na Vyuo Kusomea Taaluma Ya Udaktari Yapungua, Kilifi

Idadi ya wanafunzi wanaotuma maombi ya taaluma za udaktari kutoka kaunti ya Kilifi imeshuka kwa kiwango cha juu.

Akizungumza katika chuo cha mafunzo ya udaktari cha KMTC mjini Kilifi mkurugenzi wa vyuo vya KMTC nchini Prof Michael Kiptoo amesemaasilimia kubwa ya wanafunzi katika chuo hicho ni wa kutoka kaunti zengine.

Naye katibu wa elimu katika kaunti ya Kilifi ambaye pia ni mwenyekiti wa bodi ya elimu  Prof Gabriel Katana ameutaja ukosefu wa hamasa katika shule za upili,pamoja na itikadi za kijamii kama changamoto zinazochangia kudorora kwa idadi hiyo.

Show More

Related Articles