HabariK24 TvSwahiliSwahili VideosVideos

Ubabe unanukia tena baina ya asasi za Bunge na Mahakama

Idara za bunge na mahakama zinaelekea kuzozana tena baada ya mahakama kuu kutupilia mbali sehemu mbili za sheria inayowakinga dhidi ya kupokezwa maagizo ya mahakama wakiwa bungeni na maeneo mengine kunakoandaliwa shughuli za bunge kama hitaji la kujiwasilisha kujibu mashtaka yanayowakabili mahakamani.

Jaji wa mahakama kuu John Mativo ametupilia mbali sehemu ya 7 na ile ya 11 ya sheria hiyo iliyotiwa saini na Rais Uhuru Kenyatta mnamo Julai tarehe 21 mwaka jana na kusema zinakanganya kwa mujibu wa mwamko mpya wa katiba.

Show More

Related Articles