HabariMilele FmSwahili

Serikali yaweka mikakati kabambe kuinuia viwango vya elimu ya kiufundi nchini

Serikali imeweka mikakati kabambe ya kuinuia viwango vya elimu ya kiufundi nchini. Naibu rais William Ruto anasema mikakati hiyo inajumuisha kubuniwa upya mtaa wa elimu hiyo. Kadhalika serikali inanuia kuwawezesha wanafunzi katika taasisi za kiufundi kupokea basari kwa urahisi na kupunguza karo ili kuwavutia wanafunzi wengi zaidi kujiunga na vyuo hivyo. Naibu rais amesema hayo alipokutana na wadau katika sekta ya elimu ya kiufundi wakiongozwa na waziri wa elimu Amina Mohamed

Show More

Related Articles