HabariMilele FmSwahili

Serikali yapinga madai kuwa madaktari kutoka Cuba watapokea mishahara ya juu

Serikali imekana madai kuwa madaktari wanaotarajiwa kuja nchini kutoka Cuba watapokea mishahara ya juu kuliko ya wenzao wa humu nchini. Katibu katika wizara ya afya Peter Tum anasema madai hayo yanalenga kuwavunja moyo madaktari wa humu nchini. Akiongea huko Kapsabet anasema madaktari hao wameahidi kufanya kazi popote nchini pasipo kujali mazingira. Anasema huduma za matibabu zinatarajiwa kuimarika zaidi katika muda wa miaka 5 ijayo.

Show More

Related Articles