HabariPilipili FmPilipili FM News

Upande Mmoja Wa Barabara Eneo La Kibarani Wafunguliwa.

Shughuli za usafiri katika barabara ya Kibarani – Changamwe zinaendelea kwa mwendo wa polepole baada ya barabara ya kuja Mombasa kufunguliwa huku ile ya kuelekea Changamwe ikisalia kufungwa.

Akiongea na meza yetu ya habari, kamanda wa polisi kaunti ya Mombasa Johnstone Ipara amesema polisi wameifungua barabaa hiyo moja ya kuja mjini Mombasa huku uchunguzi ukiendelea kabla ya barabara ya kuelekea Changamwe kufunguliwa.

Haya ni baada ya gari moshi lililobeba tanki la mafuta ya petroli kupinduka hapo jana na kutatiza shughuli za usafiri katika barabara hiyo kwa muda.

Show More

Related Articles