HabariMilele FmSwahili

Lilian Mbogo na Richard Ndubai wajiondoa afisini kufuatia sakata ya bilioni 10 ya NYS

Katibu wa maswala ya vijana katika wizara ya mipango jinsia na vijana Lillian Mbogo Omollo amejiondoa kufuatia sakata ya shilingi bilioni 10 katika shirika hilo. Mkurugenzi mkuu wa NYS Richard Ndubai pia amejiondoa. Taarifa kutoka ikulu imedhibitisha kuwa rais Uhuru Kenyatta ameridhia uamuzi wao wa kujiuzulu kwa miezi mitatu ili kuruhusu uchunguzi kufanyika kuhusiana na sakata hiyo. Taarifa hiyo pia inasema rais Kenyatta anamtarajia afisa mwengine yeyote anayehusishwa na sakata hiyo kujiondoa. Kadhalika rais Kenyatta ameelezea imani katika uchunguzi unaoendelea huku pia akiagiza kufunguliwa mashitaka wahusika iwapo watapatikana na hatia.

Show More

Related Articles