HabariPilipili FmPilipili FM News

Wazazi Waombwa Kuwa Makini Wanapowapa Watoto Vifaa Vya Kidijitali

Huku serikali ikiendelea kutekeleza mfumo wa dijitali katika sekta ya elimu wadau katika sekta hiyo sasa wametaka kuwekwe mpangilio mahsusi ili kupunguza athari za mfumo huo kwa wanafunzi.

Naibu mwenyekiti wa cha walimu nchini KNUT tawi la Kilindini Ahmed Kombo, anasema mpango wa elimu ya kidijitali ni muhimu kwa kurahisisha utendakazi shuleni, ila unapaswa  kutekelezwa kwa uangalifu ili usipoteze mwelekeo wa wanafunzi.

Kombo amewataka wazazi na walimu pia kuwa makini wanapowapa watoto vifaa vya kidijitali ili kuona kuwa haviwaharibu tabia.

Amesema licha ya vifaa hivyo kurahisisha masomo ya watoto shuleni, baadhi ya wanafunzi hutumia vifaa hivyo kuingia kwa mitandao ya  filamu za ngono

Show More

Related Articles