HabariPilipili FmPilipili FM News

Miguna atasaidia Kuwakabili Mabwenyenye Katika Kaunti Ya Nairobi, Sonko Asema.

Gavana wa Nairobi Mike Sonko amejitetea kuhusu pendekezo la kumteua wakili Miguna Miguna kuwa naibu wake akisema hatobatilisha uamuzi huo.

Katika taarifa kwenye vyombo vya habari , Sonko ametolea mfano ushirikiano wa Rais Uhuru Kenyatta na kinara wa chama cha ODM Raila Odinga , akisema Miguna pia ni mkenya ambaye pia anapaswa kusamehewa, akiongeza kuwa kiongozi huyo ambaye alifurushwa nchini miezi miwili iliyopita anaweza kusaidia  kuwakabili mabwenyenye katika kaunti ya Nairobi.

Sonko ameongeza kuwa katiba iko wazi, na kwamba inampa mamlaka ya kumteua naibu wa gavana.Hata hivyo anasema iwapo Miguna atazuiwa kuchukua wadhfa huo basi atakuwa hana budi kupendekeza jina la mtu mwengine.

Hapo jana wajumbe wa bunge la kaunti ya Nairobi wakiongozwa na Spika wa bunge hilo Betreace Elachi, walipinga uteuzi wa Miguna, na kuapa kutomuidhinisha.

Show More

Related Articles