HabariPilipili FmPilipili FM News

Mgomo Wa Wahadhri Wasitishwa.

Masomo yanatarajiwa kurejea kawaida katika vyuo vikuu vya umma  baada ya wahadhiri kusitisha mgomo wao  uliodumu kwa zaidi ya miezi 3 katika vyuo vikuu vya umma.

Wakuu wa muungano wa wadhiri UASU wakiongozwa na katibu mkuu wa muungano huo Constatine wasonga, wametangaza kuafikia mpango wa kurejea kazini baina yao na mamlaka za vyuo vikuu nchini.

Wasonga amewataka wanafunzi na wafanyikazi wa vyuo vikuu kurejea kazini mara moja kuanzia hii leo, kauli ambayo imeungwa mkono na wakuu wengine wa muungano huo.

Kati ya yaliomo katika mwafaka wa kurejea kazini ni kwamba wahadhiri watasitisha mgomo wao uliodumu kwa siku 78,kusiwe na kuhangaishwa kwa wanachama wa UASU kwa sababu ya kushiriki mgomo,na pia kufanywe mageuzi kwa mtaala wa vyuo vikuu ili kuwafidia wanafunzi kimasomo kwa kipindi ambacho wamekosa masomo.

Show More

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published.