HabariMilele FmSwahili

Mchakato wa kuangazia upya marupurupu ya kustaafu ya watumishi wa umma waanzishwa

Serikali imeanza mchakato wa kuangazia upya marupurupi ya kustaafu ya watumishi wa umma. akizungumza katika mkutano na wafanyikazi wa serikali waliostaafu waziri wa Leba Ukur Yattani amedokeza kuwa jopo kazi maalum limebuniwa kuangazia maslahi yao ikiwemo kuwawezesha kunufaika na mpango wa utoaji huduma bora za afya kwa wote nchini. Yattani kadhalika anasema serikali itaidhinisha kubuniwa chama cha watumishi wa umma wanaostaafu karo ambacho kitapewa jukumu la kutoa ushauri na kuhusika katika kutatua migogoro baina ya wafanyikazi na waajiri. Naye mdhamini wa chama cha Kapro seneta , Mohamed Yusuf Haji amezitaka serikali kuu na za kaunti kuwahusisha watumishi waliostaafu katika maswala mbali mbali ya usimazi kutokana na tajiriba na uzoefu wao.

Show More

Related Articles