HabariMilele FmSwahili

Serikali yasitisha kutoa malipo katika NYS kufuatia sakata ya bilioni 9

Serikali imesitisha shughuli ya kutoa malipo katika shirika la huduma kwa vijana nys hadi uchunguzi wa madai ya kutoweka zaidi ya shilingi bilioni 10 utakapokamilika. Waziri wa utumishi wa umma na masuala ya jinsia na vijana profesa Margret Kobia, aidha anasema watakaopatikana walihusika katika sakata hiyo watachukuliwa hatua za kisheria.

Akifika mbele ya kamati ya Leba inayoongozwa na mbunge wa Bure ali Wario, Kobia alitakiwa kwanza kuweka wazi iwapo madai haya yamedhibitshwa.Wabunge nao wakisema itakuwa vigumu kuidhinishwa bajeti zaidi kwa wizara hiyo kutokana na ripoti za ufisadi.

Hata hivyo waziri Kobia ametetea wizara yake akisema tayari wametangaza kusitishwa malipo yoyote kwenye nys hadi uchunguzi huo ukamilike.Pia ameahidi hatua za kisheria kuchukuliwa watakaopatikana walihusika.

Mbali na masuala ya bajeti, kamati hiyo pia inamhoji waziri Kobia kuhusiana na ununuzi wa basi za abiria zinazohudumu jijini.

Show More

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published.