HabariMilele FmSwahili

Mwanamme azuiliwa baada ya kuwajeruhi wanawe 3, Malava kaunti ya Kakamega

Mwanamme mmoja anazuiliwa na polisi baada ya kuwajeruhi kwa kuwakata wanawe 3 katika eneo la Malava kaunti ya Kakamega. Mkuu wa polisi huko Malava Peter Mwanzo anasema mshukiwa kwa jina Johnson Mwema ambaye ni mfanyibiashara aliwavamia wanawe mkewe alipokuwa ameenda kwa hafla ya matanga na kusalia na watoto. Anasema mshukiwa ambaye anazuiliwa amekiri kosa hilo na kuwa uchunguzi zaidi unaendeshwa. Watoto hao wanatibiwa katika hospitali ya Malava.

Hata hivyo mkewe ameomba kutokamatwa kwa mumewe anayesema alifanya hivyo kutokana na matatizo ya kiafya aliyo nayo.

Show More

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published.