HabariPilipili FmPilipili FM News

Wakaazi Wa Tanariver Waanza Kuyahama Makazi Yao Kufuatia Mvua Kubwa.

Huku mvua zikiendelea kunyesha Wakazi katika kaunti za Tanariver na Garisa  wameanza kuyahama makazi yao kufuatia tayadhari ya serikali kwamba huenda Bwawa la masinga likavunja kingo zake na kusababisha mafuriko eneo hilo.

Katika kaunti ya Tanariver wenyeji wameitaka serikali kuwatafuta suluhu la kudumu, ikizingatiwa kuwa hii sio mara ya kwanza wao kuyahama makazi yao kwa sababu ya mafuriko.

kufikia sasa zaidi ya watu 160 wamefariki na maelfu ya wengine kuachwa bila makao katika maeneo mbali mbali nchini, kutokana na mafuriko ya Mvua inayoendelea kunyesha.

Show More

Related Articles