HabariPilipili FM News

Walimu Zaidi ya Elfu Nane Kuajiriwa Na TSC.

Tume ya kuajiri walimu nchini TSC inapania kuajiri jumla ya walimu 8,672 ili kufanikisha sera mpya ya serikali ya kuhakikisha wanafunzi wote wanaomaliza shule za msingi wanajiunga na shule za upili.

Walimu hao wanatarajiwa kujazilia upungufu wa zaidi ya walimu laki moja unusu katika shule za msingi na upili za umma.

Kulingana na mkurugenzi mkuu wa TSC Nancy Macharia walimu 7,672 watatumwa katika shule za upili na wengine elfu moja wakitumwa katika shule za msingi za umma.

TSC pia imeomba shilingi bilioni 8.3 kutoka kwa serikali ili kuiwezesha kusajili takriban walimu 12,626 wa shule za upili kila mwaka kwa kipindi cha miaka minee

Show More

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published.