HabariPilipili FmPilipili FM News

Wendeshaji Wa Boda Boda Kupokea Mafunzo Ya Uwekezaji

Wizara  ya utamaduni na maendeleo ya jamii  kaunti ya Kwale imeweka mikakati ya kuhamasisha  waendeshaji wa bodaboda  jinsi ya kuwekeza  ili waweze  kujiendeleza kimaisha .

Waziri wa utamaduni Kwale  Ramadhan Bungale anasema wahudumu wa sekta hiyo wanauwezo mkubwa wa kuboresha maisha yao na uchumi wa kaunti hiyo ila wamekosa kupewa mwelekeo ufaao ikilinganishwa na kaunti nyinginezo humu nchini.

Bungale ameonyeshwa kusikitishwa uhalifu unaohusishwa na wahudumu wa sekta hiyo katika kaunti ya kwale, na kutoa changamoto kwa viongozi husika kuweka mikakati ya kuthibiti hali hiyo.

Show More

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published.