HabariPilipili FmPilipili FM News

Waumini Wa Dini Ya Kiislamu Waanza Mfungo Wa Mwezi Wa Ramadhani Leo

Waumini wa dini ya kiislamu wanaanza mfungo wa mwezi mtukufu wa ramadhani leo baada ya mwezi kuonekana katika sehemu mbali mbali nchini ikiwemo hapa Mombasa.

Kadhi mkuu Sheikh Ahmed Shariff Muhdhar amethibitisha kuonekana kwa mwezi katika sehemu tofauti hapa Mombasa. Ametaka usalama uimarishwe mwezi huu haswa kwa waumini wanaotekeleza ibada za usiku.

Saum ya mwezi mtukufu wa Ramadhan ni nguzo ya nne katika dini ya kiislamu ambapo mtu huhitajika kujizuia kula na kunywa pamoja na mambo maovu ndani ya siku 29 au 30 zijazo.

Pilipili FM tunawatakia waislamu wote Ramadhan Karim wa swaum maqbul.

Show More

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published.