HabariPilipili FmPilipili FM News

Miguna Miguna Kuwasili Nchini Alasiri

Kulingana na maafisa wa tume ya kitaifa ya haki za binadam KNHRC , Miguna ambaye alifurushwa nchini mara ya pili mwezi uliopita atawasili nchini mwendo wa saa kumi jioni.

Hata hivyo bado haijabainika iwapo ataruhusiwa kuingia nchini au la, ikizingatiwa kuwa hivi majuzi, Miguna alidai kuwa bado hajakabidhiwa paspoti yake ya Kenya.

Mwishoni mwa juma msemaji wa serikali Erick Kiraithe, alishikilia kuwa ni lazima Miguna azingatie sheria na mahitaji yote ya usafiri, kabla ya kuruhusiwa kuingia humu nchini.

Show More

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published.