HabariMilele FmSwahili

Wakili Miguna Miguna kurejea nchini leo

Kizaa zaa kinatarajiwa wakati wakili na mwanasiasa Miguna Miguna akitarajiwa kurejea nchini leo. Miguna ambaye alifurushwa nchini kwa mara ya pili mwezi Machi mwaka huu anatarajiwa kuingia nchini kupitia uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta leo usiku hata hivyo serikali imeshikilia kuwa wakili Miguna Miguna hataruhusiwa kuingia bila kufuata sheria. Wikendi iliyopita msemaji wa serikali Erick Kiraithe alimtaka kuzingatie sheria na mahitaji yote ya usafiri. Hata hivyo huyo anaituhumu serikali kwa kudinda kumkabidhiwa paspoti yake ya Kenya, hata licha ya mahakama awali kuagiza arudishiwe stakabadhi hiyo muhimu.

Show More

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published.