HabariSwahili

Mshukiwa mkuu wa mauaji wa mlima Elgon Timothy Kitai ‘Cheparkach’ amekamatwa

Hatimaye mshukiwa sugu wa ujambazi aliyekuwa akisakwa vikali na polisi  kiasi cha  kuwekewa kitita cha shilingi milioni moja  kwa yeyote yule atakaye mpata timothy kitai almaarufu Cheparkach amejisalimisha kwa polisi.
Cheparkach alijisalimisha katika kituo cha polisi cha Eldoret mwendo wa saa kumi hapo jana na kufikishwa hii leo katika makao makuu ya upelelezi na jinai  jijini Nairobi ambapo hadi sasa anafanyiwa uchunguzi katika maafa yaliyotiokea katika mauwaji  mlima Elgon ambapo takriban watu  34 aliaga dunia.

Show More

Related Articles