HabariMilele FmSwahili

Sammy Kirui ,John Gakuo na washukiwa wengine 2 wa sakata ya makaburi, Mavoko wahukumiwa miaka 3 gerezani

Aliyekuwa wakati mmoja katika iliyokuwa wizara ya serikali za wilaya Sammy Kirui na aliyekuwa katibu wa jiji la Nairobi John Gakuo wamehukumiwa kifungi cha miaka 3 kuhusiana na sakata ya shilingi milioni 283 ya sakata ya ununuzi wa ardhi ya makaburi eneo la Mavoko. Pia wameagizwa kulipa faini ya shilingi milioni moja kila mmoja baada ya kupatikana na hatua ya matumizi mabaya ya afisi kwa kukosa kuzingatia sheria za uagizaji. Hakimu Dougals Ogoti pia aliwapata na hatia washtakwia wengine wawili aliekuwa mshauri wa masuala ya sheria baraza la jiji Mary Ngethe na Alexander Musee, na kuwahukumu kifungo sawia. Hata hivyo Ngethe atalipa faini ya shilingi milioni 52 au kutumia kifungo kingine cha mwaka mmoja huku Musee akitozwa faini ya shilingi milioni 32 au kifungo kingine cha mwaka mmoja zaidi. Pia walipatikana na hatia ya kutoa taarifa za uongo kuhusiana na ununuzi wa ardhi hiyo.

Show More

Related Articles