HabariPilipili FmPilipili FM News

Wanaharakati Wataka Waajiri Kutenga Mda Rasmi Wa Kunyonyesha.

Serikali imetakiwa kuhakikisha kinamama wenye watoto wanatengewa nafasi na mda wa kutosha kuwanyonyesha watoto wakiwa kazini.

Wanaharakati wa kutetea maslahi ya kina mama wenye watoto pia wanataka waajiri wote washurutishwe kutenga sehemu za kunyonyeshea watoto katika makampuni, ikiwemo kutenga dakika 30 kwa kila saa moja kwa kinamama wanaonyonyesha. Serikali za kaunti pia zimetakiwa kutenga maeneo salama ya kunyonyeshea watoto  katika sehemu za umma.

Haya ni baada ya kubainika kuwa kinamama wamekuwa wakidhalilishwa katika siku za hivi punde, ambapo ni juzi tu mama mmoja alikatazwa kunyonyesha mtoto katika mkahawa mmoja jijini Nairobi.

 

 

Show More

Related Articles