HabariMilele FmSwahili

Bi Kenyatta ataka taasisi ya familia kulindwa

Mama wa taifa Bi Margret Kenyatta amesisitiza haja ya kulindwa taasisi ya familia. Akizungumza wakati wa maadhimisho ya siku ya familia katika ukumbi wa KICC hapa Nairobi, Bi Kenyatta anasema lazima akina mama na watoto walindwe kwani ndio kiungo muhimu wa familia. Ameelezea haja ya kuwepo sera muhimu kuhusu ajira kwa wazazi ili kudumisha umoja wa familia.

Akitambua mikakati na sera iliyowekwa na wizara ya Leba kuwatambua wakongwe na watu wenye changamoto ya ulemavu kwenye familia, Bi Kenyatta anasema ipo haja ya kuimrishwa zaidi miopango hii.

Show More

Related Articles