HabariMilele FmSwahili

Kina mama jijini Nairobi waandamana kushinikiza haki ya kunyonyesha

Serikali imetakiwa kubuni sera na kuweka sheria ambayo itawawezesha akina mama wanaowanyonyesha wanao kufanya hiyo bila vikwazo katika maeneo ya umma.wakiandamana hapa jijini, kushtumu tukio la kuzuiwa mwanamke mmoja kumnynyesha mwanawe, waharakati na watetezi haki za akina mama wanasema haki zao msingi zinakiukwa kwani hakuna sehemu maalum ambazo zimetengwa kwao kuwanyonyesha watoto wao.

Ni maandamano yalioanzia bustani ya Uhuru, na kuelekea wizara afya hadi hoteli ya Olive hapa jijini ambako mama mmoja alizuiwa kumnyonyesha mwanawe, wahanarakati na akina mama wakiwa na ujumbe mmoja.Wamesuta usimamizi wa hoteli hiyo kwa kumdhalilisha mama huyo wakisema haki zake zilikiukwa.

Sasa wanataka kuwepo sheria itakayowalinda akina mama wanaonyonyesha na kujengwa maeneo maalum ya kuwawezesha kuwapa wanao haki yao.

Usimamizi wa hoteli hiyo ukaomba radhi kufuatia tukio hilo, akina mama hao wakitaka kuharakishwa mchakato wa kulinda haki zao.

Show More

Related Articles