HabariPilipili FmPilipili FM News

Shughuli Za Masomo Za Simama Kwa Wiki Mbili Mfululizo Katika Shule ya Msingi Ya Changamwe.

Viongozi eneo la changamwe sasa wanaitaka tume ya kuajiri walimu nchini TSC kusikiliza kilio cha wazazi wa shule ya msingi ya changamwe cha kutaka aliyekuwa mwalimu mkuu wa shule hiyo Fstus Njiru aendelee kuhudumu katika shule hiyo.

Hii ni baada ya mwalimu huyo kuhamishwa hadi katika shule ya msingi ya spaki hapa mombasa hali ambayo imeibua mtafaruku miongoni mwa wazazi.

 

Wazazi katika shule hiyo wamesisitiza kwamba hakuna shughuli za masomo zitakazoendelea hadi Mwalimu Njiru arudishwe shuleni humo.

Mwenyekiti wa Bodi ya Shule hiyo Mark Omondi, ameishutumu Tume ya hudma za walimu nchini TSC kwa kumhamisha mwalimu huyo , hata baada ya kuhudumu shuleni humo kwa muda wa miaka mitatu , na kupandisha kiwango cha elimu ambapo shule ya msingi ya changamwe ilikuwa ya pili bora kwa shule za msingi za umma kaunti ya mombasa.

 

Show More

Related Articles