HabariMilele FmSwahili

Hisia mseto zazidi kutolewa kuhusu madaktari kutoka Cuba kuwasili nchini

Hisia mseto zinazidi kutolewa kuhusu madaktari kutoka cuba wanaotarajiwa nchini tarehe 28 mwezi huu. Gavana wa Tana River Dhadho Godana anakiri imekuwa vigumu kwa madaktari wa humu nchini kuhudumu katika maeneo ya mashinani kaunti hiyo akisema wengi wamekuwa wakijiondoa. Mbunge wa Kiharu Ndindi Nyoro pia anasema kuja kwa madaktari hao kutakuwa na manufaa makubwa kwa wakenya.

Kwa upande wake mbunge wa Kitutu Chache Richard Onyonka ana mtizamo tofauti akitaka madaktari wa humu nchini kupewa kipau mbele.

Show More

Related Articles