HabariPilipili FmPilipili FM News

Watu Wanao chelewa Kuamka Wako Katika Hatari Ya Kufa Mapema, Utafiti Waashiria.

utafiti wa hivi karibuni uliokagua tofuati za kiafya kati ya watu wanaoamka kuchelewa na wale wanaorauka, umeonyesha hali sio nzuri sana kwa watu wanaoamka kuchelewa.

Hatari ya kifo cha mapema, matatizo ya akili na magonjwa yanayotokana na kupumua, ndio mambo yaliogunduliwa katika utaifiti huo uliounga mkono tafiti nyingine, zinazoashiria watu wanaolala kuchelewa wamo katika hatari ya kuugua magonjwa hayo.

Aidha Kila unapokuwa na uchofu zaidi ndio unajiweka katika hatari kubwa ya kuugua magonjwa kama ya moyo na mengine yanayohusu mfumo wako wa kusaga chakula.

Show More

Related Articles