HabariMilele FmSwahili

Miili 37 kati ya 45 ya waathiriwa wa mkasa wa bwawa la Patel yatabuliwa

Miili 37 kati ya 45 ya waathiriwa wa mkasa wa bwawa la Patel huko Nakuru imetambuliwa. Familia za waliowapoteza wapendwa wao zinaendelea kutambua miili hiyo katika hifadhi ya Nakuru ambapo serikali inasema itagharamia shuguli zote za mazishi. Mshirikishi wa serikali kanda ya bonde la ufa Mwogo Chimwanga anasema shuguli za kuwasaka waathiriwa zaidi inaendelea kwa ushirikiana wa maafisa kutoka shirika la msalaba mwekundu na wanajeshi.
Yakijiri hayo serikali ya kaunti ya Nakuru ikishirikiana na shirika la msalaa mwekundu zimezindua nambari maalum ya kuchangisha fedha kuwasaidia waathiriwa wa mkasa huo. Gavana Lee Kinyanjui anasema fedha zitakazochangishwa zitatumika kuwasaidia waathiriwa kuanza upya maisha yao

Show More

Related Articles