HabariMilele FmSwahili

Waziri Kariuki : Hakuna kisa chochote cha Ebola nchini

Hakuna kisa chochote cha Ebola kimegunduliwa nchini tangu ugonjwa huo kuripotiwa katika Jamuhuri ya Congo. Waziri wa afya Sicly Kariuki anasema zaidi ya maafisa 100 wa afya wametumwa katika mipaka yote na viwanja vya ndege. Akizungumza katika uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta alipozuru kutathamini viwango vya tahadhari, Bi Kariuki amekariri kujiandaa kwa serikali kukabili ugonjwa huo iwapo utazuka kama anavyotujuza

Hakikisho la waziri wa afya Sicly Kariuki kuhusu ugonjwa wa Ebola nchini baada ya visa kadhaa kuripotiwa katika jamuhuri ya Congo. Kariuki anasema zaidi ya maafisa 260 wamesambazwa kote nchini kutathmini hali.Ameongeza baraza la huduma za afya limebuniwa kufuata kwa karibu hali ya afya nchini kusaidia utambuzi wa haraka wa kirusi hicho

Kariuki aliyezuru uwanjwa wa JKIA,amedhibitisha kuendelea ukaguzi kwa raia wanaoingia nchini kupitia mipaka na viwanja vya ndege

Kwa upande wake waziri wa utalii Najib Balala amedhibitisha kupokea taarifa kutoka drc kuhusu hali ya Ebola kudhibitiwa Tayari ugonjwa huu umepelekea maafa ya watu 17 kule DRC. Ebola husababishwa na virusi kwa jina homa ya Hemoraji. Dalili zake ikiwa kufuja damu aidha kwa kutapika au kuharaka au kutoka mapuani na mdomoni. Mara nyingi husishwa na wale wanaolenda kumla popo

Show More

Related Articles