HabariMilele FmSwahili

Watu 41 wafariki kufikia sasa kufuatia mkasa wa bwawa la Patel,Nakuru

Watu 41 wamefariki hadi kufikia sasa na wengine 41 kuachwa na majeraha kufuatia mkasa wa bwawa la Patel kuvunja kingo zake kule Solai kaunti ya Nakuru. Watoto 21 ni miongoni mwa walioripotiwa kufariki. Waziri wa usalama wa ndani Dr Fred Matiangi anasema watu wengine 37 wametibiwa na kuruhusiwa kuenda nyumbani huku 4 wakisalia hospitalini. Kadhalika Matiangi amewaagiza machifu na manaibu wao kuanza usajili wa watu wasiojulikana walipo ili kupata idadi kamili ya waliofariki kwenye mkasa huo.

Matiangi amedhibitisha malori ya serikali yanayobeba chakula, dawa na mavazi na malazi kwa waathiriwa yameanza kuwasili eneo hilo anasema kila mwathiriwa atasaidika

Show More

Related Articles