HabariPilipili FmPilipili FM News

Watu 20 Wafariki Baada Ya Bwawa Moja Kuvunja Kingo Zake, Kaunti Ya Nakuru.

Idadi ya watu waliofariki baada ya bwawa la Patel katika eneo la Solai kaunti ya Nakuru kuvunja kingo zake imefika 20.

Aidha juhudi za uokoaji zinaendelea huku watu wengine wengi wakihofiwa kufunikwa na matope.

Wakaazi sasa wanaitaka serikali kubomoa mabwawa mengine mawili katika eneo hilo wakihofia janga lingine.

Gavana wa Nakuru Lee Kinyanjui anasema mabwawa hayo yatakaguliwa asubuhi hii kauli ambayo hata hivyo imeonekana kutopokelewa vizuri na wakazi hao.

Show More

Related Articles