HabariPilipili FmPilipili FM News

Jumba La Poromoka Mwembe Tayari.

Watu wawili wamethibitishwa kujeruhiwakatika eneo la mwembe tayari jijini mombasa baada ya jumba moja kuporomoka..

Akithibitisha tukio hilo Mkuu wa idara ya upekuzi wa kaunti yaani Inspektorate Mohamed Amir anasema kati ya mafundi  zaidi ya 100 waliokuwa wakiendeleza ujenzi wa jengo hilo, ni wawili tu waliojeruhiwa.

Kulingana naye shughuli za ujenzi kwa sasa zimesitishwa na eneo hilo kufungwa , huku uchunguzi ukianzishwa kubaini chanzo cha mkasa huo.

 

Show More

Related Articles